SPURS, DORTMUND, BILBAO ZAFANYA POA EUROPA LEAGUE


Son Heung-min 
Tukianzania nchini uingereza Timu Tottenham Hotspurs imenza vema kwenye mechi yake ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kuishushia kichapo kizito timu ya FK Qarabag cha goli 3-1 kwenye uwanja wake wa White hate lane.

Qarabag ndio iliyokuwa ya kwanza kuziona nyavu za tottenham baada ya kupata mkwaju wa penati kunako dakika ya 7 kupitia ka mchezaji wake Almeida de Oliveira. lakini tottenham walisawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa korea kusini Son Heung-min katika dakika 28 na dakika ta 30 kabla ya Erick Lamela kuipatia spurs goli la 3 dakika ya 86.

Na tukielekea nchini ufaransa timu ya Bourdex ya nchini humo ilibana mbavu jogoo la jiji la Liverpool kwa kutoka sare ya goli 1-1 kwenye mtanange uliopighwa katika dimba la  Stade Bordeaux-Atlantique.

Na timu ya Borrusia Dotmund ya nchini Ujerumani ikiwa katika dimba lake Signal-Iduna-Park, imetoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Krasnodar.

Dortmund walipata mabao yao kupitia  M. Ginter kwenye dakika 45,  pamoja na Joo-Ho Park kwenye dakika ya 90. ikitoka nyuma goli moja bila lililofungwa na P. Mamaev wa krasnodar kunako dakika ya 12.

michezo mingine ilizikutanisha timu za Atheltico Bilbao ambayo ilipata ushindi wa goli 3-1 dhid ya FC Augsburg, wakatio rubin kazan ikifumuliwa goli 2-1 kutoka kwa FC Sion.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment