Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini TASWA, kwa Kushirikiana na Baraza la Michezo Tanzania BMT, Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo kimetangaza kusogeza mbele sherehe ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete hadi oktoba 12 tofauti na tarehe ya awali iliyopangwa kufanyika oktoba 8 mwaka huu.
Hafla hiyo mahususi kwa ajili ya kumtunuku Rais Kikwete pia itakuwa na zoezi la kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 waliofanya vizuri kwenye michezo mbalimbali katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa rais Kikwete.
Akizungumzia na waandishi habari wa jijini DSM katibu mkuu wa Taswa, Amir Mhando amesema kuwa hafla hiyo imeahairisha kutokana na Rais kikwete na kugubikwa na shughuli nyingi za kikazi.
Kuhusiana na maandalizi ya hafla hiyo Mhando amesema kwa kiasi kikubwa yamekwisha
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment