Hali ya usalama inazidi kuwa tete katika baadhi ya miji
nchini Somalia kutokana na mashambulizi yanayoendelezwa na kundi la
wapiganaji wa Al-Shaabab ambao wameripotiwa kuteka miji miwili kusini
magharibi mwa nchi hiyo.
Mashambulizi ya hivi karibuni yalilenga wanajeshi wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani nchini humo - AMISOM, ambapo wiki iliyopita wanajeshi 37 wa AMISOM waliuawa kumi na wawili kati yao wakiwa ni kutoka Uganda.
Habari kutoka nchini Somalia zinasema vikosi vya AMISOM vimeanza kujiondoa kwenye baadhi ya miji hususan iliyokuwa ngome za Al-Shaabab kutokana na kuzidiwa nguvu.
Hata hivyo taarifa hizo hazijathibitishwa na AMISOM ingawa imethibitisha wapiganaji wa Al-Shaabab wameongeza mashambulizi na kuwarudisha wapiganaji wake nyuma.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment