RAIS WA BURKINAFASO APINDULIWA NA WALINZI WAKE


Rais wa Burkina Faso Michel Kafando (kushoto) Na Luteni Kanali Isaac Zida, katika sherehe ya kupeana madaraka, Novemba 2014, Ouagadougou. 

Serikali ya mpito nchini Burkina Faso imevunjwa baada ya kikosi cha usalama cha walinzi wa rais nchini humo kutangaza mapinduzi ikiwa ni wiki kadhaa kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Oktoba 11 mwaka huu.

Mapinduzi hayo yametangazwa baada ya viongozi wa serikali hiyo akiwemo rais Michel Kafando, waziri mkuu Isaac Zida na mawaziri kadhaa kuzuiliwa na kikosi hicho kinachohusisha walinzi wanaomtii aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Blaise Campaore aliyeondolewa madarakani mwaka 2014 kwa njia ya mapinduzi.

Habari zinasema tayari mwanachama wa kikosi hicho Jenerali Gilbert Diendere ametajwa kuwa kiongozi mpya wa mpito.Licha ya kutangaza mapinduzi kikosi hicho kimesema mipaka yote ya nchi imefungwa huku amri ya kutotoka nje ikiwekwa ili kuhakikisha hali inakuwa tulivu.
 
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment