HABARI NJEMA; MGAO SASA BASI TANZANIA KUANZIA KESHO

 

Shirika la umeme Tanzania Tanesco limesema zoezi la uingizaji gesi katika mitambo ya umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es salaam limekamilika.

Kukamilika kwa zoezi la kuingiza gesi katika mitambo hiyo ya umeme kutawezesha kuwashwa kwa mitambo mitatu ambayo itatumia umeme wa mega watts 90.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa tanesco mhandisi Felchesmi Mramba amesema zoezi la kuwashwa kwa mitambo hiyo litakuwa ni la awamu kutokana na mitambo hiyo kuwa mipya na inaanza kutumia gesi kwa mara ya kwanza na kwamba litakamilika septemba 30 mwaka huu.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment