KUELEKEA UCHAGUZI MKUU CONGO;UN YATAHADHARISHA KUHUSU USALAMA


Umoja wa mataifa umetahadharisha juu ya hali ya usalama nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo - DRC, ambako hali ya kisiasa inaripotiwa kuyumba katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwakani.

Katika ujumbe wake kwa Congo - DRC, umoja huo wa mataifa kupitia kwa mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani nchini humo Martin Kobler, umesisitiza umuhimu wa serikali ya rais Joseph Kabila kuhakikisha inasimamia kikamilifu katiba ya nchi pamoja na kuweka mazingira ya uchaguzi huo kufanyika kwa uhuru na haki.

Tahadhari hiyo inatolewa wakati, tayari rais Kabila akituhumiwa kutaka kubadili katiba ili kuendelea kubaki madarakani hatua inayotishia kuzuka kwa vita katika nchi hiyo ambako hali ya usalama ilisharejea na kuwafanya watu waliokuwa wameyakimbia makazi yao wakati wa machafuko ya nyuma kurejea.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment