VODACOM YAZINDUA DUKA JIPYA KARIAKOO #DSM


Kampuni ya Vodacom Tanzania imefungua duka  lake jipya katika eneo la Uhuru jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusogeza huduma za mandao huo karibu na wateja wake.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo, Mbunge wa Jimbo la Ilala Musa Azan Zungu amewataka wananchi wa eneo hilo kutumia kikamilifu huduma zinazotolewa na duka hilo, ili kurahisisha mawasiliano yao.

Aidha Zungu ameitaka Kampuni ya Vodacom kuendelea kulipa Kodi kwa wakati kwa Manufaa ya Maendeleo kwa wakazi na wananchi wanaoishi katika Jimbo la Ilala
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Ian Ferrao amsema duka hilo litachangia fursa kwa  utoaji wa ajira sambamba na usambazaji wa Huduma Bora za Kampuni yao.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment