CHEKI KAULI YA MAKAMU M/KITI NCCR ALIYETUHUMIWA KUTAKA KUMUUA JAMES MBATIA

 
Makamu Mwenyekiti chama cha NCCR -Mageuzi tanzania bara Leticia Mosore , amepinga utaratibu uliotumika kumwondoa madarakani kwa madai kuwa anatumika katika kukihujumu chama pamoja na kupanga njama za kutaka kumdhuru mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia.

Bi Mosore amesema uamuzi huo umekiuka kanuni na taratibu zilizo ndani ya katiba ya chama hicho hivyo mpaka sasa yeye bado ni makamu mwenyekiti wa chama hicho pia ni mwanachama halali na kuhusu tuhuma za kupamga njama za kutaka kumdhuru anaviachia vyombo vya usalama vifanye kazi yake.

Uamuzi huo umetolewa jijini dar es salaam mbele ya waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa yeye binafsi haridhishwi na namna ambavyo makubalianao ya vyama vinavyounda ukawa yanavyotekelezwa ,ambapo amesema anasikitishwa na namna ambavyo mwenyekiti wa chama hicho kutotoa ushirikianao kwenye kampeni hususani kwenye ngome za chama hicho.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment