
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mgombea ubunge wa jimbo vunjo kupitia chama cha TLP Agustino Lyatonga Mrema, amesimamisha msafara wa mgombea urais kupitia ccm Dk. John Pombe Magufuli na kumuombea kura kwa wanavunjo ili achaguliwe kuwa rais.
Tukio hilo limetokea wakati mgombea urais wa ccm dokta magufuli akiwa wilaya ya marangu katika jimbo la vunjo ,ambapo mrema alisimamisha msafara wa mgombea huyo na kupanda juu ya gari analolitumia dokta magufuli , na kumuombea kura kwa wanavunjo ili kumchagua dokta magufuli huku chama cha TLP wakiwa wamesimamisha mgombea kwa nafasi hiyo ya urais Mackmilian Lyimo .
Dokta magufuli ambaye leo ameomba kura ili aweze kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano katika maeneo ya rombo, karatea, himo, mwanga na gonja , akiwa karate eneo ambalo ni mpakani mwa Tanznaia na Kenya , dokta magufuli ameahidi kudumisha mausiano baina ya Tanznaia na Kenya katika Nyanja zote zilizomo kwenye mikataba ya jumuiya ya afrika mashariki , itakayotoa fursa na kuwapa uhuru wa kibiashara wananchi waishio mipakani.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment