UMEME WAZIDI KUWA JANGA #TZ KIDATU HATARINI, BAADA YA MTERA KUZIMWA JANA


Siku moja baada ya shirika la umeme nchini Tanesco kutangaza kuzima mitambo ya kuzalisha umeme katika bwawa la Mtera, hali si shwari katika bwawa la Kidatu mkoani Morogoro ambako wakati wowote uzalishaji wa umeme utasimama.

Meneja  wa kituo hicho cha kidatu mhandisi Justus Mtolera, amewaambia waandishi wa habari waliotembelea bwawa hilo kuwa,  mashine tatu kati ya nne za kuzalisha umeme tayari zimezimwa na moja pekee ndio inayofanya kazi kwa wakati huu.

Amesema hali hiyo imesababishwa na kupungua kwa kina cha maji katika bwawa la kidatu ambalo linapokea maji kutoka bwawa la mtera, bwawa ambalo maji yake yamepungua na kusababisha mitambo yake yote kuzimwa.

Amefafanua kuwa kwa kawaida kina cha maji katika bwawa la kidatu ni mita za ujazo 450 kutoka usawa wa bahari, lakini kina hicho kimeshuka hadi mita za ujazo 441.85 kikikaribia kina cha mwisho cha mita za ujazo 443 hivyo kuwezesha mashine moja pekee kufanya kazi

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment