TAHADHARI KWA WANANCHI KUHUSIANA NA ELNINO (MUHIMU)


Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na Mvua kubwa za El nino zinazotarajiwakunyesha katikati ya mwezi huu hadi December mwaka huu, ambazo zinaweza kusababisha athari kubwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini..

Mkuu wa kitendo cha Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia General Mbazi Msuya akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm amesema Mvua hizo zinazotarajia kunyesha kwa wingi , zinatokana ongezeko la joto katika bahari ya hindi pamoja na Mgandamizo kutoka bahari ya mediteranian.

Amesema kutokana na tishio hilo la Mvua za El nino wananchi wametakiwa kuanza kuchukua tahadhari ya kuondoka kwa wale wanaoishi mabondeni au kando za mito,pamoja na Kusafisha Mifereji katika maeneo ya makazi ili kurahisisha maji kupita .


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment