Watu sitini na mmoja wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa katika kipindi cha mwezi Septemba mwaka huu kufuatia ghasia na machafuko yanayoendelea kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangii.
Mamlaka nchini humo zimesema licha ya vifo na majeruhi hao, mamia ya watu wameyakimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo zilizoibuka baada ya kijana mmoja wa kiislamu kuuawa, hatua iliyosababisha mashambulizi ya kidini ya kulipiza kisasi.
Takwimu hizo zimetolewa wakati tahadhari juu ya uwezekano wa nchi hiyo kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na machafuko hayo ambayo yamesababisha pia uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika wiki mbili zijazo kusogezwa mbele.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment