Watu kadhaa wameuawa na wengine mamia wamejeruhiwa baada ya jengo la hoteli linalotumiwa na serikali ya Yemen katika mji wa bandari wa Aden kushambuliwa kwa makombora.
Habari zinasema miongoni mwa waliouawa ni wanajeshi wa jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia katika mashambulizi ya anga dhidi ya waasi wa Houthi.
Mwezi Julai mwaka huu, vikosi vitiifu kwa serikali ya Yemen viliukomboa mji huo muhimu wa Aden ambao kwa sasa umegeuzwa kuwa mji mkuu wa muda baada ya mji mkuu Sanaa kuangukia mikononi mwa waasi wa Houthi.
Mapigano makali yameripotiwa kuongezeka nchini Yemen kati ya vikosi vya rais Abd Rabbo Mansur Hadi na waasi wa Houthi na washirika wao wanayemuunga mkono rais wa zamani Ali Abdallah Saleh.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment