Mcheza tenis nambari moja kwa ubora duniani kwa upande wanawake Serena Willians Ametinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano Us Opens kwa kumshinda ndugu yake Venus Willians ambae ni nambari 23 kwa ubora duniani kwa seti mbili kwa moja huko Mjini Newyork Marekani
Serena mwenye miaka 33 alianza vema katika seti ya kwanza kwa ushindi wa 6-2 lakini Venus alirejea katika seti ya pili na kumshinda Serena kwa 6-1, seti ya tatu ndio ilimuhakikishia Serena kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa tabu wa 6-3.
Katika hatua ya nusu fainali mmarekani huyo atapambana na Roberta Vinci ambae ni raia wa italia katika mchezo unaotarajiwa kufanyika alhamisi ya wiki hii nchini marekani.
Endapo Serena atafanikiwa kunyakua taji hilo la Us opens atakuwa mmrekani wa kwanza kushinda mataji makubwa manne Grand Slam kwa mwaka mmoja ikiwemo FRENCH OPENS , Australia Opens, pamoja na Wimbledon ambayo ameshashinda tayari.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment