Timu ya soka taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 inatarajia kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mpambano wao wa kirafiki dhidi ya kombaini ya vijana wa mkoa huo waliochini ya miaka 15 ikiwani sehemu ya maandalizi mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya afrika chini ya umri miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2017 Madagascar.
Akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho afisa habari wa shirikisho la mpira wa miguu nchini 'TFF' Baraka Kizuguto amesema timu hiyo tayari imekwishacheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Morogoro ambapo sasa inakwenda Tanga na baada ya hapo itaelekea Arusha kwa ajili ya maandalizi kulingana na programu ya mwalimu wa kikosi hicho.
Afisa habari huyo amesema lengo la ziara hizo ni kuwawekea mazingira ya kujiamini vijana hao huku wakiwatengenezea mfumo rasmi wa kuelewana katika uchezaji pamoja, huku wakirahisisha kupata orodha ya wachezaji watakaojiunga na kikosi hicho chini ya kocha wake mkuu Bakari Shime.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment