Kiongozi wa chama ACT- wazalendo Bwana Zitto Zuber Kabwe amewaomba radhi wapiga kura wake kufuatia baadhi ya vyombo vya habari mkoani tabora kuripoti kiongozi huyo amingiza itikadi za kidini wakati akizungumza waumini wa kilutheri mkoani tabora mapema wiki hii.
Zito amewaomba radhi wanachama na wapiga kura wa chama hicho kwa kuandika ujumbe kupitia ukarasa wake wa instagram uliomaanisha kuwa kiongozi hatumiii itikadi za kidini kukiombea kura chama chake bali ana imani kuwa ana nguvu ya kuwashawishi watanzania bila kuangalia dini zao.
Aidha kiongozi wa ACT wazalendo ameandika kuwa hakumaanisha walutheri wampigie kura mlutheri mwenzao bali alitumia usemi kueleza ukweli kwamba hakuna mliutheri ambae alishawahi kuwa rais wa tanzania tangu ipate uhuru.
Katika hatua nyingine Zitto amedai kuwa hizo ni njama zinazofanywa na baadhi ya watu ili kupingana na harakati za chama hicho wakiwa na sababu zao binafsi
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment