DSTV YAZINDUA CHANELI MPYA YA BURUDANI "MAISHA MAGIC BONGO"

MMB
Kampuni ya Multichoice Tanzania imezindua chaneli mpya ijulikanayo kama "MAISHA MAGIC BONGO" itakayokuwa mahususi kwa vipindi, muziki, filamu na kazi zingine za wasanii wa Tanzania.

Chaneli hiyo mpya itakayokuwa ikionekana kwenye king'amuzi cha DSTV kwenye channel namba 160 katika itakuwa ikionekana katika mataifa yote ya bara la Afrika yaliyounganishwa na DSTV jambo litakalorahisisha kazi za wasanii wa Tanzania kuonekana.

Wakati wa uzinduzi wa channeli hiyo jijini Dar es Salaam afisa uhusiano Multichoice, Barbara Kambogi amesema kuwa licha ya chaneli hiyo kutoa burudani kwa watanzania pia itatoa fursa kwa wasanii nchini kukuza kipato chao kufuatia kazi zao kujulikana kimataifa kupitia DSTV.
 
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
 



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment