Rufaa mbili zilizokatwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam na mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yonah kupinga adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya shilingi milion tano imegonga mwamba leo, na badala yake warufani hao wamepunguziwa adhabu na sasa watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja na kuwaondolea faini ya shilingi milioni 5
Kadhalika, mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imesema Mahakama ya Kisutu, ilikuwa sahihi kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja kwa kuwa hakuna ushahidi uliothibitisha kuhusika na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara hiyo.
Jaji Rugazia amesema hakuna ushahidi ulitolewa mahakamani kueleza namna gani washtakiwa walihusika kusababisha hasara na kwamba adhabu ya kosa hilo ilitolewa kimakosa dhidi ya washtakiwa.
Ameesema kulingana na ushahidi uliotolewa hakuna lawama kwa Mahakama ya Kisutu, kumwachia huru Mgonja dhidi ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili kwenye kesi hiyo.
Mapema Julai 6, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliwatia hatiani washtakiwa hao na kumwachia huru Mgonja.
Wafungwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya makosa 10 ya kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini na kusababisha hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment