PANYA ROAD WAZIDI KUWA KERO YOMBO



Wakazi wa Yombo relini wilayani Temeke jijini dsm wamelalamikia kuwapo kwa makundi ya vibaka na waporaji katika maeneo yao ambapo katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiendesha vitendo vya Uporaji,uvamizi katika nyumba na kuwajeruhi wananchi kwa Visu na mapanga.

Wakizungumza na  SANGUJ wakazi hao wamesema makundi hayo ya wahalifu yamekuwa yakiendesha vitendo hivyo nyakati za jioni kuanzia saa moja na kuzua hofu katika eneo hilo kutokana na ukosefu wa usalama wa kutosha.

Wamesema vitendo hivyo vimeongezeka katika siku za hivi karibuni hasa kutokana na ukosefu wa umeme ambapo katika siku nne zilizopita wananchi zaidi ya kumi na tatu walivamiwa na kuporwa na kujeruhiwa kwa visu na mapanga.

 Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment