Wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita waliokosa fursa ya kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na vyuo vya nje ya nchi vinavyotoa elimu hiyo kwa gharama nafuu kwa lengo la kutimiza ndoto zao.
Wito huo umetolewa na mwakilishi mkazi nchini wa Universities Abroad Link Tanzania Tony Kabetha ambapo amesema kwa sasa China imekuja na fursa kipekee kwa kupokea wanafunzi ambao watalipia gharama ya asilimia 50 ya gharama zote na kujiunga na darasa la lugha ya kichina kwa muda wa mwaka mmoja
Bw. Kabetha ameishauri serikali kutumia fursa hiyo kukabiliana na ufinyu wa nafasi katika vyuo pia wanafunzi washauriwe kozi za kusoma kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment