WANAMICHEZO KUMUAGA RAIS KIKWETE OKTOBA 8


Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete anatarajiwa kufanya hafla ya kuagwa na chama cha waandishi wa habari za michezo nhini Taswa ikishirikiana na wizara ya ya habari Vijana utamaduni na michezo pamoja na Baraza la michezo taifa.

Hafla hiyo ya kumuaga na Rais Kikwete mwenyewe, imepangwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam lengo likiwa wanamichezo kumuaga Rais Jakaya Kikwete kwa Mchango wake aliouonyesha katika sekta ya Michezo kwa miaka kumi akiwa madarakani.

TASWA imeona kuna haja ya wanamichezo kuagana na Rais Kikwete na kumpa tuzo kutokana na masuala mbalimbali aliyofanya kwa miaka yake 10 katika kusaidia kukuza michezo na sanaa hapa nchini, ambpo Baadhi ya mambo hayo ni serikali yake ilivyolipia  makocha wa michezo ya soka, netiboli, Ngumi pamoja na kupeleka wanariadha Nchini China, Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya kimataifa.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment