YANGA YASHIKA USUKANI AZAM, SIMBA ZAUA


Ligi kuu soka tanzania bara imeendelea leo kwa jumla ya michezo saba kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini ambapo katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam mabingwa watetezi wa timu ya Dar es salaam Young Afrikans imeifunga timu ya Tz Prisons kwa goli 3-0.

mabao ya hamis Tambwe, Mbuyu Twitte na Donald Ngoma kwenye dakika ya 28 na dakika ya 45 pamoja na dakika ya 60 yaliiwezesha yanga kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja huo wa taifa wa uliopo jijini Dar salaam.

wakati huo huo Simba wenyewe wameilaza timu ya Mgambo shooting kwenye uwanja wa mkwakwani kwa goli 2-0 huku wana lambalamba wa chamazi timu ya Azam imeibamiza Stand united kwa goli 2 kwa nunge.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na jumla ya pointi 6 huku ikiwa na hazina ya magoli 5 kibindoni.

Matokeo mengine timu ya Mtibwa sukari imeifunga toto africans ya jijini mwanza kwa goli 2-1, mbeya city yenyewe ya jijini mbeya ikibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Jkt Ruvu. wakati timu ya  mwadui chini ya kocha wake Jamhuri Kiweru julio ikiifunga Africans sports goli 1-0.wakati ndanda fc ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Coast unioni kupitia mchezaji Atupele Green.

 Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
 

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment