YANGA YAZIDI KUJIKITA KILELENI YAIPIGA 2-0 MTIBWA AZAM,SIMBA ZAUA


Klabu ya soka ya yanga imeendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya mtibwa Sugar na kufikisha jumla ya alama 15 mbele ya Azam Fc ambao wameinyuka Coastal union mabao 2-0  waliyoyapata kupitia kwa wachezaji wake Kipre Tchetche, Shomar Kapombe kwenye uwanja wake wa Azam Complex.

Magoli ya Yanga yalifungwa na mchezaji Malimi Busungu kunakom dakika ya 53 ya kipindi cha pili wakati bao la pili timu hiyo likifungwa na mshamnbuliaji wake hatari Donald Ngoma kunako dakika 89.

Wakati huohuo Vijana wa msimbazi Simba Sports Club ambao walikuwa uwanja wa taifa jijini dar es salaam ikiumana dhidi ya Stand United, walibuka na ushindi wa bao 1-0 kupitia kwa Joseph Kimwaga na kufikisha jumla ya alama 12 sawa na mtibwa na sugar wakitofautiana kwa magoli ya kufunga.

Matokeo mengi ya ligi hiyo Mgambo JKT waliwatandika ndugu zao ndugu zao wa african Sports kwa goli 1-0 lilifungwa na mchezaji wake Salum Kipaga, Mjaimaji waklitopka sare ya goli 1-1 dhidi ya Ndanda Fc wakati Mwadui ya shinyanga ikitoka sare ya bila kufungana na Tz Prisons.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment