RAIS OBAMA AMTAKA RAIS WA SYRIA KUJIUZULU KUINUSURU NCHI HIYO


Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi wa Syria Bashar Al Assad hana budi kuondoka madarakani ili vita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la dola la kiislamu IS viweze kufanikiwa.

Siku moja baada ya kutofautiana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu hatma ya Assad, Obama aliongoza mkutano hapo jana pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kujadili namna ya kukabiliana na ugaidi ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzisha kampeni ya mashambulizi ya kijeshi ya angani nchini Syria na Iraq kupambana  na kundi hilo.

Obama amesema kuwashinda wanamgambo hao wa IS kunahitaji kuwepo kiongozi mpya nchini Syria na kuwahimiza viongozi wengine wa dunia kumuunga mkono kukabiliana na wanamgambo hao. 

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment