BAN KI-MOON ASISITIZA KUENDELEZWA KWA MAKUBALIANO YA AMANI SUDAN KUSINI

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon amezitaka pande zinazokinzana nchini Sudan Kusini kuonyesha nia thabiti ya kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi uliopita, ikiwemo kusimamisha mara moja operesheni za kijeshi na kuunda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa kuhusu Sudan Kusini uliofanyika kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani katibu mkuu huyo amesisitiza umuhimu wa pande zilizosaini makubaliano hayo kuheshimu ahadi zao na kutekeleza makubaliano hayo bila kuchelewa.

Wito huo umetolewa wakati hali ya usalama nchini Sudan Kusini ikiendelea kuwa mbaya kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, tangu kuibuka kwa mapigano kati ya wafuasi wa rais wa nchi hiyo Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar mwezi Desemba mwaka 2013. 

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment