WATU 37 WAUAWA KWENYE MAPIGANO YA WAASI NA JESHI AFRIKA YA KATI


Mapigano makali yameripotiwa kati ya waasi na wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako takriban watu 37 wameripotiwa kuuawa katika siku kadhaa zilizopita kutokana na machafuko.

Imeelezwa kuwa mapigano hayo yaliibuka wakati wanajeshi hao wa umoja wa mataifa walipokuwa wakiondoa vizuizi vilivyowekwa na waasi kwenye barabara ya kutoka uwanja wa ndege ili kumzuia rais wa mpito Catherine Samba Panza kuingia mjini Bangii.

Habari zinasema wanajeshi hao walishambuliwa na waasi wa kundi la anti balaka waliokuwa wameweka vizuizi hivyo hatua iliyowalazimu na wao kujibu mashambulizi.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment