BAADA ya shoo ya Tamasha la Serengeti Fiesta
2013 jijini Dar kusimama kwa muda leo alfajiri kwa hitilafu ya umeme,
inatarajiwa tena kuendelea tena saa 9 alasiri leo katika Viwanja vya
Leaders Club jijini Dar es Salaam bila kiingilio chochote.
Akizungumza na
baadhi ya mashabiki wa tamasha hilo waliokuwepo viwanjani hapo baada ya
hitilafu kurekebishwa, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,
Ruge Mutahaba alisema kuwa shoo itaendelea saa 9 mchana wa leo na
wasanii ambao hawakupata fursa ya kutumbuiza kama Nasibu Abdul 'Diamond
Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa Mitego
na Bendi ya Twanga Pepeta watatoa burudani ya nguvu saa 9 mchana wa leo
bila kiingilio chochote kile.
Mashabiki wote
ambao mlikuwa na hamu ya kuwaona baadhi ya wasanii ambao hawakutumbuiza
kutokana na hitilafu ya umeme wategemee 'sapraiz' kibao wakati wa shoo
hiyo. Wasanii waliopiga shoo baada ya umeme kurudi katika hali yake ni
pamoja na Kalapina, Chid Benz na Darasa japo mashabiki wengi walikuwa
wameondoka viwanjani hapo.
Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa Tamasha hilo Sebastian Maganga anawaomba mashabiki wote
mfike kwa wingi ili muweze kushuhudia burudani hizo.
0 maoni:
Post a Comment