KIFO CHA PANZI FURAHA YA KUNGURU SOMA KILICHOMKUTA RAIS WA CAF #ISSA HAYATOU

FIFA Senior Vice President Issa Hayatou of Cameroon 
Rais wa chama cha mpira wa miguu Afrika Caf ISSA HAYATOU sasa amepewa jukumu la kuliongoza shirikisho la mpira wa miguu Duniani Fifa kufuatia viongozi wakuu wa shirikisho hilo kufungiwa kwa miezi mitatu na kamati ya maadili ya shirikisho hilo.

Hayatou ataliongoza shirkisho hilo kwa muda wa siku 90 kufuatia kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa Fifa Sepp Blatter, makamu rais Michel Platini pamoja na katibu mkuu wa shirikisho hilo Jerome Valcke kwa madai ya kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinazoikabili shirikisho hilo

Kupitia taarifa yake Rais huyo wa Caf ambae sasa ni rais Fifa kwa muda wa siku 90 amesema kuwa amekubali kukaimu kiti hichi kwa mujibu wa katiba ya shirkisho hilo mpaka atakapo chaguliwa rais mpya kwenye  uchaguzi mkuu Februari 26, mwakani huku akidai yeye kutoweka nia ya kuwania nafasi hiyo.

Hayatou ameahidi kuwa atajitolea kulitumikia shirikisho hilo, mashirikisho wanachama, Wafanya kazi, pamoja na mashabiki wa mchezo wa soka duniani pamoja na kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo kwenye tuhuma hizo zinazoikabili Shirikisho hilo

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo 
 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment