TANESCO YAZIMA MITAMBO YA UMEME BWAWA LA MTERA


Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limezima mitambo ya kuzalisha umeme katika Bwawa la Mtera lililopo mpakani mwa mikoa ya Iringa na Dodoma baada ya kina cha maji kupungua chini ya wastani, kutokana na ukame unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Meneja wa kituo cha Mtera Mhandisi Abdallah Ikwasa amewaambia waandishi wa habari waliotembelea bwawa hilo kuwa hatua imechukuliwa wiki moja sasa hali ambayo imesababisha upungufu wa umeme kwa wateja wa gridi ya taifa.

Amesema kwa kawaida kina cha maji  kwenye bwawa hilo ni mita za ujazo 698.3 kutoka usawa wa bahari na kiwango cha chini ni mita za ujazo 690 kutoka usawa wa bahari, lakini kiwango hicho kimepungua hadi mita za ujazo 687.53 kutoka usawa  wa bahari, na hivyo kutokana an ushauri wa kitaalam imelazamu shirika hilo kuzima mitambo ya kuzalisha umeme.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment