Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva.
TUMSHUKURU Mungu kwa kuwa nchi yetu ya Tanzania kwa mara nyingine tena inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25, mwaka huu tukiwa na amani, hivyo ahimidiwe daima.Nasema hivyo kwa kuwa baadhi ya vijana waliofikisha miaka 18 hivi karibuni hawajawahi kushiriki kwenye uchaguzi wowote na uchaguzi huu ni wa kwanza kwao.
Vijana hawa na watu wengine, wanahitaji kujifunza au kukumbushwa juu ya mambo ya kufanya siku ya uchaguzi ili kufanya zoezi la upigaji kura kuwa lenye mafanikio na kuepusha uvunjifu wa sheria unaoweza kumweka mtu matatani na kuvuruga zoezi lenyewe.
Kwa bahati mbaya, elimu kwa mpiga kura haijatolewa mwaka huu, jambo ninaloliona kuwa ni la hatari.
Elimu kwa mpiga kura bado inahitajika ili kila mwananchi afahamu haki na wajibu wake katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Elimu kwa mpiga kura bado inahitajika ili kila mwananchi afahamu haki na wajibu wake katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ndiyo yenye jukumu la kutoa elimu hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva anasema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni pamoja na uhaba wa asasi za kiraia zinazotoa elimu kwa wapiga kura na kuwafikia wananchi wote nchi nzima.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva anasema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni pamoja na uhaba wa asasi za kiraia zinazotoa elimu kwa wapiga kura na kuwafikia wananchi wote nchi nzima.
Anasema watatumia vyombo vya habari vikiwamo vinavyomilikiwa na taasisi za dini ili kuwafikia wananchi haraka zaidi katika kuelimisha, sasa mimi leo najitolea kutoa elimu hiyo.
Zingatia haya siku ya uchaguzi: Mpiga kura anatakiwa kufuata sheria za uchaguzi na kanuni zake.
Wahi kituoni: Jambo la msingi ni kuwahi asubuhi katika kituo cha kupigia kura kuanzia saa moja ukiwa na kadi ya kupigia kura.
Wahi kituoni: Jambo la msingi ni kuwahi asubuhi katika kituo cha kupigia kura kuanzia saa moja ukiwa na kadi ya kupigia kura.
Kila mpiga kura anatakiwa kujua kituo atakachopigia kura na kuhakiki kama jina lake lipo kwenye orodha ya wapiga kura kwenye kituo husika.Panga foleni: Ukifika kituoni panga foleni ya kuingia chumba cha kupigia kura. Zingatia vituo vitafungwa kuanzia saa 10 jioni na watakaokuwa kwenye mstari baada ya muda huo wataruhusiwa kuendelea kupiga kura mpaka watakapomaliza.
Nisisitize tu kwamba wananchi wajitokeze kwa wingi ili wawachague viongozi wao.
Kupiga kura ni jambo la muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu. Msipojitokeza kwa wingi basi msilaumu kiongozi atakayechaguliwa na wengine.
Kupiga kura ni jambo la muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu. Msipojitokeza kwa wingi basi msilaumu kiongozi atakayechaguliwa na wengine.
Usivae sare za chama: Inasisitizwa kwamba mpiga kura asivae nguo yenye nembo au alama yoyote ya chama cha siasa kwenye kituo cha kupigia kura. Kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za uchaguzi na mtuhumiwa anaweza kushitakiwa kwa kuhujumu mchakato wa upigaji kura.
Kwa hiyo, fulana, kofia, bendera au kanga au nguo yoyote inayovaliwa na chama chochote haitakiwi kwenye eneo la kupigia kura.Usilete ushabiki: Jambo la tatu, wapiga kura wasilete ushabiki kwenye vituo vya kupigia kura. Mambo ya ushabiki ni pamoja na kuongelea matokeo ya uchaguzi kabla hayajatangazwa na mamlaka husika zilizokasimiwa jukumu hilo.
Jambo hilo linajenga hisia tofauti miongoni mwa wapiga kura na linaweza kusababisha vurugu endapo matokeo yatakuwa kinyume chake.Sitarajii kuona watu wakitengeneza makundi ya kujadili mwenendo wa uchaguzi kwenye vituo. Hiyo ni sawa na kampeni siku ya uchaguzi.
Ukipiga kura nenda nyumbani: Jambo la nne, mwananchi akimaliza kupiga kura aende nyumbani kusubiri matokeo kutangazwa. Kuendelea kukaa kwenye vituo vya kupigia kura kunasababisha msongamano usio wa lazima.
Hakuna haja ya kukaa kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kulinda kura kwa sababu tayari mawakala wa vyama vya siasa watakuwepo kwa ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa uchaguzi.
Hakuna haja ya kukaa kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kulinda kura kwa sababu tayari mawakala wa vyama vya siasa watakuwepo kwa ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa uchaguzi.
Jukumu la kutangaza matokeo ya urais ni la Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Tume pia imekasimisha jukumu la kutangaza matokeo ngazi ya kata kwa msimamizi msaidizi wa kata na ngazi ya jimbo kwa msimamizi wa halmashauri.
Kuna taarifa kuwa Nec imejipanga kutangaza matokeo ya urais ndani ya siku tatu kwa sababu watatumia Mfumo wa Kusimamia Matokeo (RMS) ambao utawawezesha kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo.
Licha ya kutakiwa kisheria kutangaza matokeo hayo ndani ya siku saba, Nec imebainisha kwamba mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa matokeo kutoka sehemu mbalimbali nchini.
0 maoni:
Post a Comment