Deogratius Mongela na Chande AbdallahI
NAUMA sana! Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kata ya Mwembe Mkavu, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani, Ramadhani Mloli (37) amemuua mkewe, maarufu kwa jina la Mama wa Naironi kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili kisha na yeye kujiua kwa kisu pia.
NAUMA sana! Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kata ya Mwembe Mkavu, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani, Ramadhani Mloli (37) amemuua mkewe, maarufu kwa jina la Mama wa Naironi kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili kisha na yeye kujiua kwa kisu pia.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Agosti 21, mwaka huu, saa moja na nusu asubuhi nje ya Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), iliyopo Bagamoyo.Kwa mujibu wa chanzo, Ramadhani na mkewe huyo walitengana kufuatia ugomvi usiojulikana ambapo mke huyo alikwenda kuishi kwa ndugu zake, Kibaha, Pwani huku akiwa amefungua kesi Bakwata akidai talaka.
Chanzo kikasema kuwa, siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kwenye ofisi hizo mapema kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.Chanzo kinasema kesi hiyo ilitakiwa kusikilizwa saa tatu asubuhi, lakini ilikatishwa na tukio hilo baada ya Ramadhani kuwahi eneo hilo na kutoa kisu alichokificha na kumchoma nacho marehemu sehemu mbalimbali za mwili mpaka kukata roho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, baada ya kutekeleza mauaji hayo, Ramadhani naye alijichoma kisu huku akijikata bila huruma eneo zima la tumbo na kuutoa utumbo nje kisha akachukua mchanga na kujipakaza kwenye utumbo kabla ya kuishiwa nguvu na kudondoka chini akiwa hoi.
“Ilikuwa inatisha sana! Halijawahi kutokea tukio la aina hii hapa Bagamoyo. Haraka sana tuliwachukua na kuwakimbiza Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo. Lakini wakati huo mwanamke hakuonesha dalili ya kuwa hai,” alisema mmoja wa wasamaria wema waliojitokeza kuwapeleka hospitali.
Waandishi wetu walifika katika hospitali hiyo na kukutana na Mganga Mkuu Mfawidhi, Emmanuel Nhonoli aliyesema:
“Tuliwapokea wakiwa katika hali mbaya sana. Katika vipimo vya awali iligundulika kuwa, mwanamke alishafariki dunia lakini mwanaume alikuwa mahututi na baadaye aliaga dunia.”
Kwa mujibu wa majirani walioomba hifadhi ya majina yao, kabla ya kuachana wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara na kusababisha mwanamke huyo kuwa na mazoea ya kukimbilia kwao na kurudi hali ikiwa imetulia.
“Mpaka sasa hakuna anayejua kiundani tatizo hasa zaidi ya wao wenyewe. Ila siku moja kabla ya tukio, mwanaume alinunua kisu na kukinoa sana akisema kesho katika hukumu yao kule Bakwata atafanya kitu cha ajabu sana, hakuna atakayetegemea.
“Inaonekana Rama (Ramadhani) alikusudia kufanya mauaji haya maana kaacha ujumbe unaosema mali zake zote warithi ni watoto wake wanne huku akimtaja msimamizi mkuu kuwa ni kaka yake mkubwa aitwaye Twaha,” alisema jirani mmoja.
Naye mjumbe wa shina katika eneo la Mwembe Mkavu, Kata ya Kidongo Chekundu, Mohamed Khamis alisema:
“Yaani sijui kimetokea kitu gani ambacho kimesababisha haya. Kwa kweli tumehuzunika sana maana Ramadhani alikuwa mtu wa swala sana. Sema juzi kabla ya tukio kwa mujibu wa rafiki zake alikuwa akiongea kesho (siku ya tukio) atafanya kitu cha ajabu pale Bakwata.”
Mazishi ya marehemu hao yalifanyika Agosti 22, mwaka huu ambapo Ramadhani alizikwa nyumbani kwake huku mwanamke akizikwa Kibaha kwa ndugu zake.
0 maoni:
Post a Comment