Aliyekuwa mke wa Dk. Wilbroad Slaa amezunguza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amemtaka Dk Slaa kuwaomba radhi maaskofu wa Kanisa la Katoliki kutokana na tuhuma dhidi yao kwamba baadhi yao wanadaiwa kupokea rushwa.
Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tu tangu Dk Slaa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni za Chadema za mgombea wake wa Urais Edward Lowassa ambapo alidai kuwa aliambiwa kuwa katika kuungwa mkono kwa mgombea huyo, baadhi ya maaskofu hao walipokea rushwa ingawa hata hivyo aliweka tahadhari kuwa tuhuma hizo ni za kuambiwa, na kwamba kama ni kweli maaskofu hao watumbu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Rose Kamili amedai kuwa amesikitishwa na tuhuma hizo alizoziita za kupotosha ambazo hazina msingi na zinapaswa kupuuzwa.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment