WANAFUNZI SHULE YA GEITA WALAMIKIA KUNYANYASWA NA UONGOZI WA SHULE



Wanafunzi 31wa kidato cha kwanza na nne katika shule ya  Sekondari ya Geita  Islamic wamerudishwa nyumbani  baada ya kugoma kuingia darasani kwa kile kinachodaiwa kunyanyaswa na uongozi wa shule hiyo.

SANGUJ imeshuhudua wanafunzi hao wakiwa mtaani wakirandaranda na kudai kuwa hawana la kufanya huku wakilalamika pia kuwa hawana nauli za kuwafikisha makwao.

Wanafunzi hao wamelalamikia uongozi wa sekondari hiyo juu ya taratibu za uendeshaji wa shule  hususan tukio lilitokea  Agosti 26 mwaka huu kwa mwanafunzi wa kidato cha nne aliyetajwa kwa jina Fadhili Zuberi ambaye inadaiwa aliumizwa baada ya kupigwa kichwani na mlinzi wa kampuni mmoja na kilazimika kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment