MASHABIKI; TUNAMSHUKURU MKWASA KWA KUIKOA STARS


Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wametoa maoni tofaouti kuhusiana na timu ya taifa ya taifa stars inayonolewa na kocha mzawa Charles Borniface Mkwasa baada ya kutoshana nguvu na Nigeria kwenye mchezo wake wa kufuzu kwa michuano ya mataifa afrika afcon 2017.

Wakizungumza na SANGUJ kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kuwa wamekubaliana na kikosi hicho licha ya kukabiliwa na changamoto chache ikiwemo ya ukosefu wa mfungaji wa magoli kwa kuwa timu hiyo ilitengeza nafsi nyingi lakini hazikuzaa matunda kufuatia kukosa mfungaji wa kuaminika.

Aidha mashabiki hao wa soka wameliomba shirikisho la soka Tanzania Tff kuweka mikakati ambayo itakuwa rafiki kwa mashabiki na wapenzi wa soka nchini, ili kuwapa nafasi watanzania waliowengi kuishabikia timu yao ya taifa.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment