KAMPENI; MAGUFULI NIKIWA RAIS NITAFANYA KAZI KAMA EDWARD MORINGE SOKOINE


Mgombea urais kupitia ccm dokta john pombe magufuli amesema akiwa rais atafanya kazi kwa usimamizi thabiti wa kimaendeleo kwa kupinga rushwa,ufisadi na uzembe kazini, kama alivyokuwa anafanya kazi aliyekuwa waziri mkuu wa awamu ya tatu wa tanzania  marehemu Edward moringe sokoine.

Dk.Magufuli ambaye leo amefanya ziara ya kuomba kura mkoani arusha katika maeneo ya mto wa mbu,monduli,longido na kumalizia arusha mjini kwa kupokelewa na maelfu ya watu ,ambapo akiwa monduli aliweza kutembelea kaburi la Hayati Edward Moringe Sokoine , huku wazee wa kimila ya kimasai wakimuombea dua na baadae kushiriki katika nyimbo za kimasai.


Dk.Magufuli amesema serikali inajivunia uwezo wa kiutendaji wa hayati sokoine,ambapo  amedai endepo atachaguliwa kuwa  rais wa awamu ya tano  atahakikisha anajituma kwa kufuata nyayo zake za kiutendaji ili kuliletea taifa maendeleo.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment