Majogoo hao wa jiji la Liverpool wanatarajiwa kukamilisha makubaliano
yao siku ya Alhamisi na Klopp raia wa Ujerumani kuchukua rasmi mikoba
ya Brendan Rodgers mwishoni mwa juma hili, kwa mkataba wa miaka mitatu.
Rodgers alitimuliwa siku ya Jumapili kufuatia suluhu ya 1-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.
Klopp ameomba kuambatana na wasaidizi wake wawili wa zamani katika benchi la ufundi ambao ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Buvac
raia wa Bosnia mwenye miaka 54 na mjerumani Krawietz mwenye miaka 43,
walitoa ushirikiano mzuri na kupata mafanikio makubwa wakifanya kazi
pamoja klabuni Borussia Dortmund.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment