Klabu ya soka ya Athletic Bilbao imevunja rekodi yake ya kunyakua taji la kombe la super cup baada ya miaka 31 kwa kutoka sare ya goli 1-1 Dhdi ya barcelona kwenye mchezo wa pili wa fainali wa kombe hilo ambapo awali Barcelona ililala kwa goli 4-0.
Mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Nou camp Barcerlona ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao kwa bao maridadi kutoka kwa mchezaji hatari wa timu hiyo Lionel Messi katika dakika ya 44.
Alikuwa mchezaji mkongwe wa raia wa Hispania Aritz Aduriz aliyeisawazishia Bilbao katika dakika ya 81 na kupelekea mpaka mwisho wa mwisho wa mchezo huo timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 hjuku bilbao wakiwa na hazina kubwa ya magoli waliyopata katika dimba la San Mames Bilbao na kupeleka matokeo kuwa ya jumla bao 5-1.
Timu hizo sasa zitakutana tena kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka hispania utakaofanyika mwishoni mwa juma hili.
0 maoni:
Post a Comment