Wakati kocha wa timu ya taifa "taifa stars" charles bornface mkwasa akitaja kikosi chake cha wachezaji 22 kitakacho kwenda uturuki kwa kambi ya wiki moja atawakosa wachezaji wake wa kimataifa wanaokipiga katika klabu mbalimbali barani afrika na ulaya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Baraka Kizuguto amesema kuwa timu hiyo itawakosa baadhi ya nyota wake watano wa kimataifa akiwemo mchezaji Mbwana Samata,Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa , Hassan Seif, Pamoja na mshambuliji Haji Yusuph.
Aidha jatika hatua nyingine kizguto amesema kuwa kikosi hicho kitaweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki katika
jiji la Estanbull pamoja na kucheza michezo yake m iwili ya kirafiki ikiwemo
dhidi ya Libya pamoja na ule dhidi ya uturuki.
Kikosi hicho cha kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa inakibarua kizito dhidi ya kikosi cha Nigeria chini ya kocha wake mpya Sunday Olise September 5 mwaka huu kwa jili ya kufuzu michuano ya AFCON.
Wachezaji waliochaguliwa ni All Mustafa (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam FC), Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba SC), Juma Abdul, Haji Mngwali, Kelvin Yondani, Nadir Haroub (Yanga SC).
Viungo Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deus Kaseke (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), Washambuliaji John Bocco, Farid Musa, (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Simon Msuva (Yanga SC), na Ibrahim Ajib (Simba SC)

0 maoni:
Post a Comment