MWANARIADHA MLEMAVU OSCAR PISTORIUS KIFUNGO CHA NJE



 

Waziri wa sheria nchini Afrika Kusini amepinga uamuzi wa kuachiliwa kwa mwanariadha Oscar Pistorius.Michael Masutha ambaye ni waziri wa sheria nchni Afrika kusini amasema kuwa uamuzi wa kumuachilia mwanariadha huyo umechukuliwa mapema mno



Oscar Pistorius amekaa gerezani kwa muda wa miezi kumi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp na alitarajiwa kuachiliwa ili atumikie kifungo chake cha nyumbani kuanzia kesho



Mwanariadha huyo mwenye ulemavu raia wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake ambapo anatarajiwa kuwa huenda  akaachiliwa huru hapo kesho Agosti 21.



Kwa mujibu wa taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa na kutumikia kifungo cha nje.



Oscar alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela katika kesi iliyovuta hisia kali kote  ulimwenguni ambapo inadhaniwa kuwa alimpiga risasi mpenzi wake akidai kuwa alidhani ni wezi wanaingia kwake katika siku ya wapendanao yaani Valentines Day

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment