WABONGO WATANO WAULA ORLANDO PIRATES #SA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPDul9PDjH-HEEjAHwPMXwXcB3TaP6LAU7EJABLveaXgcSnGlYqUeFHzPjqJQkS7aBLjg8trvGFSlljuDdiQMz8qEs7Sqq39-e3fey0JEXM5mlB69AHUNHdEAQ0jrwLoh3liZ7E0gUmpfq/s1600/DSC_1206.JPG


 

Timu ya soka taifa chini ya miaka ya 15 inatarajia kuanza ziara yake ya kimataifa barani afrika mwezi desemba mwaka huu kwa ajili maandalizi ya kufudhu kwa michuano ya afrika chini ya miaka 17 itakatofanyika madagascar 2017. 

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamali Malinzi amesema timu hiyo itaanza ziara yake mwishoni mwa mwaka katika nchi za zambia , Zimbabwe, Botswana pamoja na nchi za kusini mwa Afrika

 

 

Aidha malinzi amesema kuwa TFF imeingia mkataba na kituo cha ukuzaji wa vipaji cha Alliance Sports cha jjini Mwanza kwa ajili ya kuwatunza vijana 20 waliopatikana kwenye mashindano ya Taifa chini ya miaka 15.

 

Katika hatua nyingine malinzi ameeleza kuwa shirikisho hilo limewatafutia nafasi vijana watano kujiunga  na klabu maarufu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu soka ya Afrika kusini ambao ni Assad Ally Juma (Zanzibar) Maziku Amani na Issa Abdi (Dodoma,) Kelvin Deogratius (Geita) na Athumani Maulid kutoka Kigoma.



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment