Baada ya kuishushia kichapo cha Magoli 2-1 timu ya Mbeya City, Mabingwa wa soka afrika mashariki na kati Timu ya Azam imeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Costa Unioni utakaochezwa kwenye uwanja wa Nyumbani Azam Complex.
Msemaji mkuu wa Klabu hiyo Jaffari Idd amewaambia waandishi wa habari kuwa baada ya ushindi huo muhimu, kikosi hicho sasa kimeelekeza shauku kwenye mchezo dhidi ya Wagosi wa kaya ili kuhakikisha wanaendelea kuvuna ushindi kwa kila mechi.
Aidha Jaffari amewatoa hofu mahabiki wa timu hiyo kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo kuonekana inafunga mabao machache msimu huu akidai kuwa kwenye mchezo wa soka kitu cha msingi ni alama tatu muhimu.
Kuhusiana na suala la mchezaji wa mbeya city Juma Nyosso kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshammbulaiji wa Azam John Boko, Jaffar amethibitisha kuwa klabu hiyo imepeleka malalamiko shirikisho la miguu nchini TFF k na kwamba wanaimani hatua stahiki zitachukuliwa.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment