HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA SONGEA NA RUVUMA #MAJIMAJISELEBUKA


Wanamchezo mbalimbali kutoka mkoa wa Ruvuma wanatarajiwa kushiriki tamasha lenye lengo kutambua juhudi za kiuchumi zinazofanywa na wajasiriamali wa mkoa huo maarufu kama MAJIMAJI SELEBUKA litakaloanza oktoba 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Tamasha hilo ambalo litajumuisha michezo mbalimbali ikiwemno kuendesha baiskeli na riadha, pia linalenga kuibua vipaji mbalimbali vya vijana wa mkoa wa Ruvuma ili kuweza kujitengenezea fursa mbalimbali za ajira kutipitia michezo mbalimbali.

Akizungumza na waansishi habari jijini DSM, Mratibu wa tamsha hilo Amina Mdoe amsema kuwa tamasha hilo ambalo litakuwa la wiki moja linalenga pia kusambaza elimu katika shuLe mbalimbali za mkoani Ruvuma zikiwemo shule za Sekondari Songea wavulana na wasichana, shule ya sekondari Msamala pamoja na Kigonsea.

 Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment