Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetoa tahadhari kuhusu uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko wa magonjwa, hususan yale yanayoambukizwa na mbu, ikiwemo Homa ya Bonde la Ufa, katika kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Desemba mwaka huu, kufuatia taarifa za kuwepo mvua kubwa za El Nino katika kipindi hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk.Mwele Malecela amewaambia Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam kwamba Taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani kote zinaonyesha kuwepo kwa mvua kubwa za El Nino katika kipindi cha Mwezi Oktoba na Desemba mwaka huu.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu amesisitiza kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuchukua hatua kadhaa za tahadhari sasa, ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi jinsi ya kujiepusha na ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, badala ya kusubiri mpaka mlipuko wa ugonjwa huo utakapoingia.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment