MAHAKAMA YAMALIZA KESI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI MBEYA


Mgogoro wa muda mrefu wa Wachungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi, umeingia katika sura mpya baada ya baraza la ardhi la wilaya ya Mbeya kutoa hukumu ndogo, likiamuru wachungaji watano wa kanisa hilo kuondolewa kwa nguvu katika nyumba za kanisa.

Mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha waumini  kufunga kwa minyororo Kanisa kuu la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi, usharika wa Jacalanda Jijini Mbeya , ulisababisha uongozi wa kanisa hilo  kufungua kesi ya msingi katika baraza la ardhi la Wilaya ya Mbeya kupinga tabia ya waumini kufunga kanisa hilo kila wakati.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, upande wa mashtaka ukafungua kesi ndogo  kuomba baraza hilo, liwaamuru wachungaji wanaoishi kwenye nyumba za kanisa kuziachia nyumba hizo ili zitumike kwa matumizi ya kanisa, shauri ambalo limehukumiwa na baraza hilo, kwa kuamuru wachungaji hao waondolewe kwenye nyumba hizo.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment