Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini Solly Mahlangu,amethibitisha kutumbuiza katika tamasha la kuombe amani linalotarajiwa kufanyika Oktoba 4 katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Tamasha hilo kutoka kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama,amewaambia hayo waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam alipokuwa akizungumzia maendeleo ya maandalizi ya tamasha hilo sambamba na kutaja majina ya waimbaji wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya nchi,watakao tumbuiza Oktoba 25 katika tamasha la kuombea amani
Msama,amesema,Maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri ambapo kwa mara nyingine,ameeendelea kutaja majina ya waimbaji waliokwisha kuthibitisha kutumbuiza katika tamasha hilo,ambapo mbali na Solly Mahlangu,amelitaja kundi la Kelechi kutoka nchini Uingereza kuwa limethibitisha kuja kutumbuiza katika tamasha hilo.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment