Mabingwa wa Soka Tanzania Bara,Yanga ya Dar Es Salaam,imeanza vyema kampeni ya kutetea Ubingwa ilioutwa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kuilaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-0.
Katika mchezo huo Yanga waliutawala mchezo kwa kiwango kikubwa wakiucheza mpira wao wa asili wa kuanzia pembeni huku kwa muda mwingi wakiwalazimisha pia Coastal kushindwa kushambulia lango lao kutokana kuwakabia juu katika eneo lao.
Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na Simon Msuva,akikimbia hatua 15 kutoka katikati ya kiwanja na kukutana na beki wa kati wa Coastal akiwa hana la kufanya na kutumia uzembe wa beki ya Caostal kupasiana one two na Hamisi Tambwe na bao la pili likifungwa na Donald Ngoma.
Yanga walitengeneza nafasi nyingi za kufunga huku viungo vyao vikiudhibiti vyema mchezo wao kutokana na kile kilichoonekana ubora wa timu hiyo na wachezaji kuzoeana.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment