Mjumbe wa kamati ya ushindi ya chama cha mapinduzi ccm Christopher Ole Sendeke , amewataka wanccm kudumisha amani na utulivu bila kujibu maneno ya kashfa dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa , baada ya kujua mbinu zinazofanywa na baadhi ya chama pinzani kuanzisha vurugu zitazoifanya jumuia za kimataifa kushawishi serikali ya mseto.
Mjumbe huyo wa kamati ya ushindi ya CCM, ameitaka serikali kusimamia amani na utulivu baada ya uchaguzi na kuwataka viongozi wa vyama vya upinzani kuwatayarisha kisaikolojia wanachama wao juu ya kushindwa kwa uchaguzi huo.
Akipokelewa na mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya shujaa , Mgombea urais kupitia ccm Dk. john pombe magufuli amesema ataendelea kulinda maliasili zinazopatikana katika mji wa moshi ili kuendelea kuwa mji wa kitalii ambao unaweza kuongeza ajira na pato la taifa.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment