Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imekonga nyoyo za watanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Timu ya taifa ya Malawi "the flames" katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Magoli ya Taifa stars yamewekwa nyavuni na wachezaji wakulipwa katika klabu ya Tp Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Ali Samatta aliyefunga bao la kwanza kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Thomas Ulimwengu aliyeihadaa ngome ya Malawi iliyokuwa mepoteza umakini.
Goli la pili liliwekwa wavumi na Thomas Ulimwengu aliyemalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hadji Mwinyi baada ya golikipa kuupoteza mpira kwa kushindwa kudaka mpira baada ya kuchanganyana beki wake katika na kuifanya stars kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwa hatua inayofuata.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment