MTIKILA KUAGWA KARIMJEE KESHO OKTOBAR 7 #RIPMCHUNGAJIMTIKILA



Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Democratic Patry DP Mchungaji Christopher Mtikila unatarajiwa kuagwa kesho oktober 7 katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam

Tukio hilo la kuaga mwili wa marehemu mchungaji Mtikila linatarajiwa  kuanza majira ya saa tano asubuhi ambapo viongozi mbalimbali  wa serikali, vyama vya siasa na wananchi watapata fursa ya  kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mwili huo kusafirishwa  kuelekea kijijini kwao Milo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa mazishi alhamisi wiki hii.

Akizungumza na SANGUJ nyumbani kwa marehemu mikocheni jijini DSM mdogo wa marehemu Stanely Mtikila amesema mwili utatolewa katika hospitali ya Lugalo na kufikishwa kwanza nyumbani kwake kabla ya kupelekwa katika viwanja hivyo vya Karimjee.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment