Kwanza niazne kwa kutoa
shukrani kwa mwenyezi mungu mwingi warehema kwa kutujualia afya na uzima
japo na kuna wengine ambao wapo hospatalini wakiwa wagonjwa mahututi lakini
hatuna budi kumshukuru kwa kuwa yeye ndie mpanga na muweza wa yote. Pili
nikushukuru wewe ndugu msomaji wangu ni matumani yangu huu mzima wa afya
Watu wengi huenda wakawa hawafahamu ni nini maanisha
naposema “sometimes tunahitaji maamuzi magumu ili kufikia ndoto na malengo
tuliyojiwekea katika maisha “
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yaliyotokea hapa nchini ambayo
mengi yamekuwa yakustajaabisha umma wa
watanzania, kumekuwa na matukio kama vile viongozi kuhama vyama vyao, waandishi
habari maarufu nchini, kuhama vituo vyao walivofanyia kazi kwa muda mrefu
wakiwa na malengo mbalimbali lakini matukio haya yote yametokana na watu hawa
katika kuheshimu malengo na dhamira waliyojiwekea kwenye maisha.
Sitaki kuingia kwenye siasa sababu mambo yako wazi na yanaonekana,ila
katikati ya mwaka huu tumeshuhudia mtangazaji DJ Fetty akitangaza kuacha kazi
ya utangazaji na kuamua kuendelea na maisha yake mengine ya mbali na fani hiyo
ya utangazaji. Wakati manii buyo akiwaanga wafanyakazi wenzake mtangazaji huo
alisema kunhanmuda unahitaji kufanya maamuzi ili kufikiandoto na malengo
alitojiwekea katika maisha yake.
Ni kweli hakuna mtu ambae alidhani mangazazi huyo angeweza
kukihama kituo hiko maarufu nchini licha ya kukifanyia kazi kwa muda mrefu na
kumpatia umaarufu wa hali ya juu ndani na nje ya Tanzania
Mbali na huyo mwanzoni mwa mwaka jana pia tulimshuhudia
mtangazaji mwingine maarufu nchini Maulid Kitenge aliyehama kutoka kituo
amvbacho alikifanyia kazi kwa miaka 10
kuanzia 2004 mpaka 2014 na kuamua kukihama kituo hiko ambacho kilimoa umaarufu
zaidi nchini na kuelekea kwenye kituo ambacho kilikuwa kigeni kwenye masikio ya
watu.
“Najua ni jambo gumu sana kutoka eneo ambalo umelizoea kwa
muda mrefu lakini ukweli ni kwamba nimehama nilipokuwa nikifanyia kazi awali
baada kuitumikia kwa miaka 10” hayo
maamuzi magumu ambayo aliyafanya Maulid na kuyaleza kupitia akaunti yake
twitter, ni kweli kuna ugumu Fulani kuhaa mahali ambao umepazoea lakini
inakubidi kufanya hivo endapo kama unahisi hapo ulipo huwezi kufikia ndoto zako.
Diamond Platinum ni msanii mwenye mafanikio sana Tanzania
kwa ujumla siri kubwa ya mafanikio yake mpaka kufuka hapo alipo yametokana na
kipaji chake cha uimbaji pamoja na maamuzi aliyokuwa akiyafanya ilikufikia hapa
alipo.
Watu wengi
wanajiuliza kwanini msanii huyu yupo karibu sana na Rais Kikwete kuliko wasanii
wengine nchini, kikubwa ni maamuzi
magumu aliyofanya kwa kujijengea uaminifu kwa mkubwa wa nchi.` Sitaki kueleza
sana ili kikubwa alichokifanya diamond ni kufanya maamuzi ya kujitolea kwa
kiongozi huyo kwa kutumbuiza bure baadhi
ya matukio ambayo akialikwa na kiongozi huyo,
Ni jambo gumu sana ambalo haliwezi kufanywa na msanii yoyote nchini
wengi wangeichukua nafasi hiyo kama sehemu kumaliza shida zao.
Si huyo tu wapo wasanii wengine hapa nchini ambao
wamefanikiwa kutokana na kufanya maamuzi ambayo si ya kawaida katika maisha yao
mfano Tunda Man Lina Sanga waligombana na wazazi wao wakitakiwa wawe wapenda
dini lakini kwa upande wao wote
walihitaji kuwa wasanii,
Hao ni baadhi lakini tunafahamu kwamba jkwa mila na tamaduni
za kiafrika ni jambo gumu sana kugombana na mzazi wako kwa kuyakataa yale
ambayo wanayotaka
Ni kweli sometimes tunahitaji maamuzi magumu ambayo ni
sahihi ili kufikia yale tuliojiwekea chamsingi maamuzi hayo yawe sahihipamoja
na kujikita zaidi kwenye
upande ambao tunaukimbilia na kuhakikisha tunapata mafaniko zaidi ili
kuondoa lawama, kashfa tuhuma, kejeli kutoka kwa wale waliokuwa wakitushauri.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment